Marekani na waitifaki wake wake waliiwekea Russia vikwazo vikubwa baada ya Moscow kuanzisha oparesheni ya kijeshi dhidi ya Ukraine. Marekani na washirika wake aidha zimetaka nchi mbalimbali zipunguze kutegemea gesi ya Moscow.
Marekani na washirika wake wameiwekea vikwazo Russia huku nchi za Magharibi zikihofia kwamba kuongezeka vikwazo dhidi ya Moscow katika sekta za kiuchumi na hasa sekta ya mafuta na gesi kutavuruga zaidi hali ya uchumi wa Ulaya na kusambaratisha masoko ya kimataifa ya nishati kwa ujumla.
Vikwazo anuwai dhidi ya Russia hadi sasa vimeisababishia Ulaya changamoto chungu nzima.
Rais Vladmir Putin wa Russia alisema jana kwenye mkusanyiko wa wafanyakazi wa kiwanda kimoja cha teknoljia ya masuala ya anga za mbali katika eneo la Buryatia umbali wa kiomita 4,400 mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Moscow kuwa: "Tunakabiliwa na vita na vikwazo vikubwa lakini licha ya hayo Russia imeweza kujipatia fedha za ziada za kigeni sawa na dola bilioni 332.
Putin ameongeza kuwa, kiwango cha mfumuko wa bei nchini Russia kimepungua licha ya njama zote Wamagharibi za kuiwekea nchi hiyo vikwazo. Amesema hivi sasa nchi za Magharibi zinataabika nkwa mfumuko wa bei wa juu zaidi ikilinganishwa na Russia.
342/